Amazing books that are waiting for you

Imân na Uislam

Written By : Mawlânâ Khâlıd Al-Baghdâdî
Publisher : Hakikat Kitabevi
Download Read Book
Free Of Charge  

112
page
3-4
hours
25.9k
view

Kwa usaidizi na nguvu zinazotolewa na Allah Ta’ala (Mwenyezi Mungu) mwenye kulinda ulimwengu na vilivyomo vyote, na ndiye anayetoa neema zote na zawadi na ndie asiyelala, sasa tunaanza kufafanua maneno ya Mtume wetu “Sall-Allahu ta’ala alaihi wa sallam”.

Kipenzi chetu Hadrat umar ibn al-Khattab radiya-Allahu ta’ala anhu na ambae alikuwa kiongozi shujaa wa Uisilam. Na mwenye cheo cha juu miongoni mwa masahaba zake mtume Sall-Allahu ta’ala alaihi wasallam, na alikuwa marufu kwa ukweli wake anaeleza kwamba:

Ilikuwa ni siku ambayo badhi yetu (masahaba) tulikuepo mbele ya Mtume Sall-Allahu ta’ala alaihi wa sallam, siku hiyo na mda huo ulikuwa mwenye baraka, siku yenye thaman kadir kwamba kila mtu angependa kuishi katika siku hiyo mara kwa mara akipata fursa tena. Katika siku hiyo, sote tulijaa furaha na heshima ya kuwa kukusanyika pamoja (masahaba) za Mtume na kukaa karibu nae na tukaona uso wake na maneno yake mazuri ambayo yalikuwa ni chakula cha roho na kutuliza nyoyo. Kusisitiza thamani, heshima ya siku hiyo, Masahaba waliobarikiwa wanasema: ” ilikuwa ni siku....” ni siku ambayo haikadiriki kwasababu ni siku ambayo Jibril alaihi s-salam alijitokeza mbele ya binadamu na sote tukamuona, tukapata kusikia sauti yake na kusikia elimu nzuri mtu anayopenda kujisikilizia mwenyewe kwa makini kupitia mdomo wa Rasulullah sall-Allah ta’ala alaihi wa sallam

What Readers Say? 1

Say Something...

You Might Also Like